Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imeanza kutekeleza kwa Vitendo azima ya Serikali ya kuwahimiza wananchi kutembelea Vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini ili kuewea kujionea mambo
mambo yaliyopo ndani ya nchi yetu pamoja na kujenga Uchumi wa Taifa.
Watumishi,Wakuu wa Idara na Viongozi waandamizi wa Wilaya Wametembelea hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko ndani ya Wilaya hii ili kujionea Wanyama anbao wanaopatikana katika hifadhi hiyo
Hifadhi ya Taifa ya Gombe iko mkoa wa Kigoma,Wilaya ya Kigoma kuna wanyama ambao hawapatikani kwenye kwenye hifadhi nyingine za Taifa wanyama hao ni Sokwe,ambao kwa kadri ya historia wanyama hawa ndio chimboko la Binadamu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inatoa wito kwa Watanzania wote nchini kutembelea hifadhi hii ili kujionea wanyama na Msitu mzuri.
Wote mnakaribishwa.
Near Rairway Station
Postal Address: P.O.BOX 332
Telephone: 028 28024865
Mobile: +255767210541
Barua pepe: kigomadistric@gmail.com
Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa